Hivi karibu nilikulete habari kutoka inasema kutengenezwa
kwa filamu ya My life is crime uliyogharimu pesa nyingi sana za Kenya sasa
habari kutoka Kenya ni kuwa watengenezaji wa filamu mpya yenye bajeti
kubwa kabisa Kenya, My Life in Crime kuchagua mwigizaji Jim Iyke kama mhusika
mkuu wa Kazi hiyo na kuacha waigizaji wengine wengi tu kutoka Kenya ambao
wanajulikana sana na wanafanya poa sana imekuwa gumzo ndani ya Kenya baada ya Muongozaji wa kazi hii Neil Schell ameibuka na
kutetea uamuzi wake huo.
Director huyu amesema kuwa, kazi hii ni kubwa na yenye
malengo ya kuwavuta watazamaji wengi kabisa kutoka kona mbalimbali za dunia,
kitu ambacho Jim Iyke kwa nafasi yake na uzoefu wake anaweza kukifanya kwa kazi
hii.
Pia Director huyu ameongeza kuwa, Msanii kama Jim Iyke ni
mtu ambaye amejituma kwa kazi hii baada ya kuona mwongozo wake kutokana na
kuchukua hatua kuajiri mwalimu wa kumfundisha lafudhi ya lugha na hata
kujilipia nauli ya ndege kuja Kenya kwa ajili ya usahili wa waigizaji wa kazi
hii.
Post a Comment