UBAGUZI baina ya vyama vya upinzani uliopata nguvu bungeni wakati wa kuanzisha Kambi Rasmi ya Upinzani chini ya Chadema, umeanza kutafuna chama hicho chenye ushawishi mkubwa kuliko vyama vingine vya upinzani Tanzania Bara.
Uundwaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani
bungeni, ulitokana na msimamo wa Chadema yenye wabunge wengi bungeni,
kukataa kushirikisha vyama vingine vya upinzani, ikiwamo CUF ambayo
ilikuwa na idadi ya wabunge wanaotosheleza kuunda Kambi ya Upinzani,
lakini imezidiwa kiidadi na Chadema.
Chadema pia ilikataa kushirikiana na
NCCR- Mageuzi, TLP, UDP na kuamua kuunda kambi ya wabunge wa Chadema
pekee, ambapo kwa busara kwa kuwa CUF pia ingeweza kuunda Kambi ya
Upinzani, kambi hiyo ya Chadema ikapewa jina la Kambi Rasmi ya Upinzani
bungeni.
Athari za ubaguzi huo zilijitokeza
Arusha hivi karibuni, ambapo chama hicho kilionekana kutaka kuongoza
halmashauri ya jiji hilo, lakini kikashindwa baada ya kukosa kura mbili
tu za TLP, na jana imejidhihirisha wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Katika siasa za Arusha, baada ya Chadema
kutetea viti vyake vinne vya udiwani katika uchaguzi mdogo na uliokuwa
muhimu kwa siasa za Chadema, ilifikisha viti 15 kwenye Baraza la
Madiwani la Arusha, huku CCM ikibakiwa na viti 12 na TLP viti sita.
Pia Chadema mbali na kuwa na viti hivyo
15, inayo nafasi ya kuongeza kiti zaidi, kwani kuna nafasi moja ya viti
maalumu iliyokuwa ikishikiliwa na Rehema Mohamed, aliyetimuliwa mwaka
2011.
Hata hivyo, pamoja na Chadema kuongoza
kwa kuwa na viti vingi vya udiwani Arusha, haikuwa na uwezo wa kumweka
Meya, kwa kuwa idadi ya madiwani wake ni 16 na kingehitaji zaidi ya kura
17 katika baraza, ili kupata nafasi ya kuongoza halmashauri hiyo.
Hivyo Chadema ilihitaji kushirikiana na TLP, ili kupata zaidi ya nusu ya kura inayohitajika kikanuni kumuweka Meya madarakani.
Uvinza Baada ya Chadema kusema haina
uroho wa madaraka katika umeya wa jiji la Arusha, chama hicho kimejikuta
katika mazingira kama ya Arusha, mkoani Kigoma.
Mkoa wa Kigoma, katika halmashauri mpya ya Uvinza, Chadema ikishindwa kuishawishi NCCR-Mageuzi kuwaunga mkono, itakuwa katika mazingira ya kukosa nafasi ya kuongoza halmashauri hiyo mpya.
Mkoa wa Kigoma, katika halmashauri mpya ya Uvinza, Chadema ikishindwa kuishawishi NCCR-Mageuzi kuwaunga mkono, itakuwa katika mazingira ya kukosa nafasi ya kuongoza halmashauri hiyo mpya.
Katika halmashauri hiyo, CCM ina
madiwani wanane, Chadema madiwani saba na NCCR-Mageuzi inayo madiwani
watano na Mbunge mmoja, ambaye anaingia katika Baraza la Madiwani na
anaruhusiwa kupiga kura na hivyo chama hicho kuwa madiwani sita.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge
wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) alinukuliwa akiwataka
madiwani wa Chadema na NCCR- Mageuzi, kuunganisha nguvu ili CCM iunde
Kambi ya Upinzani katika halmashauri hiyo.
“Chadema na NCCR-Mageuzi tuna madiwani
13 katika Halmashauri ya Wilaya Uvinza…CCM ina madiwani wanane tu, hivyo
tuna kura nyingi upinzani. Chadema ina madiwani saba, NCCR-Mageuzi
watano na Mbunge mmoja,” alinukuliwa Zitto akishawishi huku akisema
wakishindwa kuungana, CCM itapita katikati.
Umoja wavunjika Tofauti na matazamio ya
Zitto, kwamba vyama hivyo vingeweka mgombea mmoja dhidi ya mgombea wa
CCM, Hamisi Mkwafi, NCCRMageuzi pamoja na kuwa na madiwani sita tu,
ilisimamisha mgombea wake, Fidelis Kumbo, na Chadema ikaamua kuweka
mgombea wake, Cassiano Mabondo.
Katika mazingira yaliyoonesha kuwa vyama
hivyo vya upinzani, ikiwemo Chadema vilikuwa na uroho wa nafasi ya
Mwenyekiti, havikusimamisha mgombea katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti,
ambayo CCM ilijikuta ikiwa haina mpinzani baada ya kumsimamisha Diwani
wa Kalya, Lucas Kanoni.
Awamu ya kwanza ya uchaguzi huo uliokuwa
ukisimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza,
Nicolous Kombe na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ulishindwa
kupata mshindi baada ya kila chama kupata kura saba.
Matokeo hayo yaliamsha mjadala wa muda
mrefu na mwishowe walikubaliana uchaguzi huo urudiwe, ambapo matokeo
yake yalionesha kuwa wajumbe walipigia kura wagombea wa vyama vyao kwani
mgombea wa CCM, aliongoza kwa kupata kura nane na kufuatiwa na mgombea
wa Chadema aliyepata kura saba na wa NCCR -Mageuzi aliambulia kura sita.
Utata Baada ya matokeo ya uchaguzi wa
raundi ya pili, mjadala uliibuka tena kuhusu matakwa ya kikanuni, kwamba
mshindi anapaswa kupata zaidi ya nusu ya kura za wajumbe waliopiga
kura, ambazo ni 11, jambo ambalo hakuna mgombea hata mmoja aliyefikisha.
Msimamizi wa Uchaguzi, Kombe alilazimika
kusitisha mjadala huo kwa muda, ili wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi
wapate ufafanuzi wa kisheria, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Baada ya zaidi ya saa moja ya kusubiri,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Miriam Mbaga,
alisema majibu waliyopata yanaeleza kuwa aliyeshinda kwa kura nyingi,
mgombea wa CCM Mkwafi, anapaswa kutangazwa mshindi.
Majibu hayo ya Mkurugenzi yalizua
tafrani ambapo baadhi ya madiwani walimtaka Mkurugenzi huyo kufuta kauli
hiyo, kwa madai kwamba si kauli rasmi.
Mkurugenzi huyo alilazimika kufuta kauli
hiyo, na baadaye Msimamizi wa Uchaguzi, Kombe aliahirisha uchaguzi huo
hadi utakapoitishwa upya.
source: MPEKUZI
Post a Comment