Dar es Salaam. Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi jana alikuwa na wakati mgumu
katika Kongamano la Amani lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), baada ya Katibu Mkuu wa Chadema,
Dk Willbroad Slaa kumtaka ajiuzulu
kutokana na kushindwa kudhibiti uhalifu nchini.
kutokana na kushindwa kudhibiti uhalifu nchini.
Mbali ya Dk Nchimbi, Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi
katika kongamano hilo, Brigedia Jenerali, Elias Athanas naye alibanwa
akitakiwa kueleza tuhuma za askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ), kuhusishwa na vitendo vya ubakaji na utesaji wa raia mjini
Mtwara.
Akizungumza katika kongamano hilo, Dk Slaa alisema
hakuna haja ya kutafuta mchawi wa amani ya nchi bali, Serikali inapaswa
kulaumiwa kutokana na watendaji wake kushindwa kuwajibika ipasavyo.
Alitoa mfano wa kitendo cha Bandari ya Dar es
Salaam kutumiwa kupitisha pembe za ndovu wakati maofisa polisi wakiwemo
ni kitendo cha aibu ambacho kinatosha kumfanya Waziri Nchimbi ajiuzulu.
Akijibu madai hayo wakati akihitimisha kongamano
hilo, Waziri Nchimbi alikiri kuwa baadhi ya polisi wamekuwa na tabia ya
kujihusisha na rushwa na katika kupambana na hali hiyo, Serikali
imeshawatimu kazi askari 101 katika kipindi cha mwaka 2012.
Hata hivyo, Dk Nchimbi alisema suluhisho la
matatizo yaliyopo ndani ya Jeshi la Polisi siyo kuwatimua kazi askari
pekee na ndiyo maana Serikali imeanza mkakati wa kutoa mafunzo ya
maadili ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa weledi.
Alisema ataendelea kupokea changamoto kutoka kwa
wadau wote wa amani na kupongeza waliobuni kongamano hilo, huku akiahidi
kutoa ushirikiano kufanikisha jambo lolote linalohusiana na mjadala wa
amani ya nchi.
Kuhusu ubakaji na utesaji wa wanajeshi, Dk Slaa
alisema inasikitisha kuona jeshi ambalo linapaswa kulinda amani linatesa
na kuwabaka raia.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa
CUF, Julius Mtatiro ambaye alisema anao ushahidi wa wanachama wa chama
chake waliojeruhiwa na kupakwa pilipili akisema kwamba jeshi hilo
limekuwa na baadhi ya askari wakatili tofauti na misingi ya kuanzishwa
kwake.
Akijibu tuhuma hizo, Brigedia Jenerali Athanas
alikanusha madai hayo akisema siyo kweli kwamba JWTZ linaendesha unyama
na kwamba lipo Mtwara kwa ajili ya kulinda amani na kusema tuhuma hizo
ni za mitaani.
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alidai kuwa
tangu nchi ilipopata uhuru haijawahi kuwa na amani ya kweli akitoa
mfano wa wananchi kuhamishwa kwa nguvu katika maeneo yao.
Alisema katika siku za karibuni, tofauti na zamani
polisi ilipokuwa ikifanya kazi ya kudhibiti uhalifu, sasa inaonekana
kama kazi yake ni kudhibiti upinzani na limekuwa likituhumiwa mara kwa
mara kwa kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na kusababisha mauaji.
Alipiga kijembe akisema kwamba CCM kinakaribia kuanguka na ndiyo maana kimekuwa kikitumia mabavu kudhibiti upinzani.
Alipiga kijembe akisema kwamba CCM kinakaribia kuanguka na ndiyo maana kimekuwa kikitumia mabavu kudhibiti upinzani.
Awali, Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Gaudence Mpangala alisema amani inaweza kutoweka ikiwa CCM kitaendelea
kutumia dola kudhibiti upinzani.
Alisema CCM kinapaswa kufanya kazi kama ilivyo
vyama vingine vya siasa na kuonya kwamba hata kukiwa na makongamano
mengi, amani haitapatikana kama hakitajitathmini na kuchukua hatua.
Alisema polisi imekuwa ikifanya makosa kuzuia
maandamano ya vyama vya upinzani akisema sheria iko wazi ikisema
vinachotakiwa kufanya ni kulitaarifu jeshi hilo kuhusu ratiba ya
shughuli zake.
Post a Comment