Wananchi wakiwa wamenyosha mikono juu kuunga mkono hatua ya mbunge Msigwa na Chama cha Chadema kuja na wazo la kupinga kodi katika line za simu
Wananchi wakiwa wametulia kusikiliza maneno matamu ya mbunge Msigwa
Mbunge Msigwa akisikiliza swali kutoka kwa mwananchi
Mbunge Msigwa akimbembeleza mwananchi kuulizwa swali baada ya kupanda jukwaani na kushindwa kuuliza swali kwa madai kuwa swali lake limepotea njiani wakati akipanda jukwaani kutokana kuona aibu umati mkubwa wa wananchi
Mkazi wa Iringa Maneno Mbuma akiuliza swali kwa mbunge
Mheshimiwa mimia sina swali naomba kuomba ridhaa ya wananchi kuonana na wewe faragha ili tuongee faragha
Wakazi wa Kihesa waliofika katika mkutano huo
Uchangiaji wa ujenzi wa ofisi ya kata ya Chadema
MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa ( Chadema) amewataka wananchi wa jimbo la Iringa mjini kujiandaa kujaza fomu maalum za kupinga uamuzi wa serikali ya CCM chini ya waziri wa fedha Dr Wiliam Mgimwa kutaka wamiliki wa simu kuanza kulipia kodi ya Tsh 1000 kwa kila kadi (line) ya simu .
Mbunge Msigwa ametoa wito huo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja wa ofisi ya kata ya Kihesa mjini hapa.
Alisema kuwa Chadema hakipotayari kuona serikali ya CCM ikiendelea kuwakandamiza wananchi wanyonge kwa kuwawekea kodi katika line zao za simu jambo ambalo alisema ni mzigo kwa mtanzania na kuwa kamwe suala hilo watalipinga kwa nguvu zote na kuomba wananchi kujiandaa kujaza fomu maalum ambazo zitaanza kupitishwa katika mikutano yake itakayoanza hivi karibuni .
Mbunge Msigwa alisema tayari zoezo kama hilo amelianza mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika na kuwataka wananchi wa Iringa kujitokeza kwa wingi katika mikutano yake ambayo itakwenda sambamba na kupinga uamuzi huo kandamizi wa serikali wa kutoza kodi katika line za simu.
" Nawaombeni mara baada ya kuanza zoezi hilo la kujaza fomu kila mmoja ashiriki kwa kujaza jina lake na namba yake ya simu ili kupeleka fomu hizo bungeni kupinga uamuzi huo ambao umepitishwa na wabunge wa CCM "
Post a Comment