Warembo hao ambao walikuwa wakitokea Sinza kuelekea
Manzese, Dar walivamiwa na vijana hao ambao wengi wao ni waendesha
pikipiki maarufu kama bodaboda, walipokaribia Makutano ya Barabara ya
Shekilango na Morogoro, Dar.
“Kila siku wanapita hapa wakiwa nusu utupu, sasa leo
tumewakomesha, serikali inatangaza Ukimwi ni hatari, wao hawajali,
wanatutia majaribuni,” alisikika akisema mwendesha
bodaboda mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa waliowavamia wasichana
hao.
Baada
ya warembo hao kuelezwa hivyo akina dada hao hawakufurahishwa na maneno hayo na
badala yake
wakawaporomoshea matusi mazito madereva hao, hali
iliyowafanya wapandwe na hasira.
“Madereva wale baada ya kusikia wakitukanwa waliwavamia
wasichana hao na kuanza kuwachania nguo kwa maelezo kwamba
badala ya kuwa nusu utupu, ni vema wakakaa uchi wa mnyama
kabisa.
Post a Comment