Gazeti la mwanachi limeripoti kwamba Tume ya Vyuo Vikuu
Nchini (TCU) imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo
vikuu kwa kutumia uzoefu wao ambapo udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo
2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na
kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.
Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo
Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na
kufaulu kwa wastani wa daraja B ambapo Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu
ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia Mwananchi kwamba baada ya
kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu lakini
wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo
maalumu.
Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of
Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo
kama wanavyofanya watahiniwa wengine, Sifa zinazotakiwa ili kujiunga…. mwombaji
anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu
isiyopungua darasa la saba, atakiwa kuwa
na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia
kukisoma, awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo
inayotumika kufundishia vyuoni”
Mkurugenzi amekaririwa akisema “Kuna watu wameishia
darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa
mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu, mfumo huu utawawezesha kuendelea
na masomo bila tatizo, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu ambayo mtahiniwa
ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja
B, daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni
50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.
Post a Comment