UJIO NA UTAMBULISHO WA "aloysonTv" www.youtube.com/aloysontv

ITAZAME VIDEO HII HAPA CHINI


aloyson.com Inapenda kuitambulisha "aloysonTv" itakayokuwa ikiwakusanyia na nkuwaletea matukio ya picha mwendo (video) katika habari nyingi ambazo aloyson.com watakuwa wakiyaripoti.

Pia kwa nia ya dhati kabisa inapenda kukitambulisha kipindi cha MY ZONE kitakachokuwa kikifanya vipindi mbalimbali kwa watu maarufu na wasio maarufu ili kuleta uwiano wa habari zisizopata wasaha mzuri wa kuwafikia watu wengi.

aloysonTv, imevutiwa zaidi na kuguswa kuhakikisha inapata habari zaidi za wazee ambapo katika ulimwengu huu wa teknolojia iliyokuwa kwa kiasi kikubwa na kuwasahau sana. Tutapata kujua nini hasa wazee wetu huvutiwa na ulimwengu huu, nini wanavutiwa toka kwa vijana na pia fashion zinavyotofautiana hasa kwa vijana na wazee toka enzi hizo na za sasa na mengine mengi yanayojiri miongoni mwao.

Hii yote inaambatana na kutambua umuhimu wa wazee wetu waliotuleta na kutulea sisi ambao ndiyo vijana na nguvu kazi ya sasa na tunaohitajika kama tegemezi kwao.

OMBI KWA WADAU WA HABARI:
Msaada wenu unahitajika sana katika kusaidia yale yote mazuri ambayo jamii inastahili kufikiwa. Bila nguvu ya ushirikiano wenu sitaweza kuyatimiza haya yote na hivyo basi kwa dhati kabisa nawaomba kutoa msaada kuzisambaza habari hizi ikiwa ni nguvu kazi na ubunifu wa vijana tunaopenda kujituma na kuitumikia jamii kwa maendeleo jamii yetu ya Tanzania.

MWISHO:
Shukrani za dhati ni kwa M/Mungu na kwenu wanahabari, wadau wa habari na wasomaji au wafuatiliaji wa habari, heshima za dhati sana kwenu nyote na Mungu awejalie mema mengi.
 Aloyce Mlawa || Aloyson mmiliki wa aloyson.com
Juma Omary || Omry, Director of Photography.

Imeandikwa na;
Aloyce Mlawa,
(Aloyson)
Blogger
www.aloyson.com
aloyson@live.com

Post a Comment

 
Top