Zenani Mandela
Makaziwe Mandela
Watoto wa rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela,wameamua
kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi wake watatu kutoka katika makampuni
anayoyamiliki.
Makaziwe na Zenani Mandela wanadai kuwa watatu hao hawana
haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani ya dola
milioni 1.1. Kesi hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu afya
ya Mandela mwenye umri wa miaka 94.
Mandela aliondoka hospitalini baada ya kutibiwa ugonjwa
wa mapafu pamoja na homa ya mapafu, na katika rekodi amelazwa hospitalini mara
ya nne katika kipindi cha miaka miwili.
Duru zinasema kuwa kumekuwa na mzozo wa kichinichini
tangu mwaka 2005 wa kudhibiti pesa zinazotokana na mauzo kwenye jina la Mandela
hususan picha alizokuwa anachora akiwa jela.
Post a Comment