Muigizaji amabe anafanya vizuri sana kwenye tasna ya
bongo movie pia mmiliki wa kampuni ya Endless film Wema Sepetu baada ya kumpa
kajala shavu la kufanya kazi ndani ya kampuni yake amesema yeye kama Wema
sepetu hategemei Kajala kujakufanya kazi katika kampuni ili kumlipa zile million
kumi na tatu 13 alizomsaidia ili asiingie jela
Wema sepetu aliongea kwenye kipindi cha XXL, Wema amesema
Kajala atakuwa akifanya kazi zake lakini atakuwa akimlipa kama kawaida. Ambapo
Kajala kwa sasa atacheza filamu moja inaitwa Princess Sasha ambayo atacheza
kama mhusika mkuu kwenye filamu hiyo.
“Tutaenda kuishoot nje ya Dar, ninataka kuishoot mandhari
fulani hivi kama ya kijijini. Ni mtoto wa mfalme, Kajala ndo atakuwa Princess
Sasha, she is going to be the main character, “ alisema Wema.
Kajala naye amesema aliamua kujichora tattoo ya jina la
Wema kwasababu anamchukulia kama shujaa.
“Mi naweza kusema nimeichora kuonesha nimeappreciate vipi
kitu alichonifanyia , watu wengine wanaichukulia vibaya, wataongea vibaya,
lakini mimi najua moyoni mwangu. Sababu nimeona siwezi kumlipa hiyo hela sasa
hivi.
Ntamkumbuka siku zote hata chochote kikitokea atabakia
kuwa mtu… yaani she is my hero.”
Post a Comment