Mpanda Katavi
Jeshi la polisi mkoa wa Katavi limemkamata Hilali Abdalah (30) mkazi wa mtaa wa majengo mjini hapa kwa kumkamata akiwa na vifaa vya kutengenezea noti bandia akiwa katika nyumba ya kulala wageni Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema Hilali alikamatwa hapo jana majira ya ssa 8 mchana katika nyumba ya kulala wageni inaitwa Ambassodor aliyoko katika mtaa wa mji wa zamani Kata ya kashaulili mjini hapa
Alisema mtuhumiwa alikamatwa kufuatia taarifa za kiitelejensia kulifikia jeshi la polisi mkoa wa Katavi kutoka kwa raia wema kuwa Hilali anajihusisha na shughuli hiyo ya utengenezaji wa noto bandia Kidavashari alivitaja vifaa aliwavyo kamatwa navyo mtuhumiwa kuwa ni karatasi ngumu 217 ambazo hutumika kutengenezea noto bandia za shilingi 10,000 bomba mbili za sindano zenye dawa maalumu kwa ajiri ya kubadilishia rangi ya karatasi hizo ili zifanane na pesa hizo
Alivitaja vifaa vingine kuwa ni powder chupa moja kwa ajili ya ya kumfanya mteja ataakizishika mapema zisiacche alama ya vidole kwenye pesa beseni moja jeusi kwa ajiri ya kusafishia karatasi hizo mara baada ya kuzipitishia kwenye hatua kadha
vifaa ningine alivyo kamatwa navyo Hilali ni karatasi 21 plain kwa ajiri ya kufunikia karatasi ngumu zisipate hewa wakati wa utengenezwaji wa noti bandia soltap 2 kwa ajiri ya kubania karatasi zisipate hewa mapema pasi moja ya umeme kwa ajili ya kukaushia pesa hizo mara baada ya kuziosha na ugolo vijiko vitatu ambao alikuwa akiutumia kama kilevi wakati akifanya shughuli hiyo haramu
Kamanda waa polisi mkoa wa Katavi alieleza awali mtuhumiwa alikuwa akijishughulisha na shughuli za kuuza mitumba kaika soko la Buzogwe mjini hapa na baadae alihamia mkoani Tanga na ndiko aliko patia ujuzi wa kutengeneza noti bandia
Kidashari alieleza hatimaye baada ya kupata utaalamu huo alirejea Mpanda na kuanza kazi hiyo mbaya ya kuvunja sheria za Nchi Alisema katika maelezo yake ya awalialikiri kufanya shughuli hiyo kwa kile alicho kieleza ni kutokana na yeye hapo siku za nyuma aliwahi kutapeliwa pesa kwa kupewa noto bandia ndio maana ameamua na yeye kulipa kisasi kwa watu wengine
Pia mtuhumiwa alitaja sababu nyingine kuwa ni katika kujitafutia maisha kwa njia ya ytafuataji ndio maana akaamua kujitafutia pesa kwa njia hii mtuhumiwa anategemewa kufikishwa mahakamani mara upelelezi wa kesi hii utakapo kamilika ili aweze kujibu mashitaka yanayo mkabili
Post a Comment