Hit maker wa ngoma isiyochuja masikioni ‘Si uliniambia’ MB Dog ameushangaa mfumo wa muziki wa Tanzania akilinganisha na mfumo wa muziki wa nchi kadhaa alizozitembelea na kikubwa alichokiona ni kwamba Tanzania hakuna ‘Respect’ kwa wasanii waliotangulia ama waliofanya vizuri na sasa wamenyamaza.
MB Dog amefunguka katika exclusive interview aliyofanya na leotainmenttz kuwa kwa nchi nyingine alizotembelea wasanii waliofanya vizuri miaka flani ya nyuma halafu wakanyamaza hupewa heshima hata kwenye matukio ya kimuziki tofauti kabisa na Tz ambapo aliyepo mbele ndo yupo na aliyemnyamaza hayuko kwenye hesabu.
“Yaani system ambayo mimi naiona ambayo iko juu sana kwa wenzetu, kitu kikubwa kwanza ni respect ya watu ambao waliotangulia na wanaofuata, unajua hapa muziki wa kitanzania kitu cha kwanza yaani aliyekuwepo mbele ndiye yupo, aliyenyamaza basi hayuko kwenye hesabu.
Kitu ambacho kinafanya tunashindwa kusaidiana kwa sababu watu wanatutengeneza tunakuwa wazito, mimi ambae nilikuwa siiimbi mfano nina issue nyingine lakini nilikuwa na nguvu ya kuweza kumsaidia mtu flani, lakini kutokana na system ambayo iko ya Tanzania ambayo inafurahisha yaani mtu akishawezeshwa kidogo akishapanda wanamtengenezea kitu ambacho hawezi kupata msaada kutoka kwa mtu flani au akishakuwa mtu flani anawekwa mbele ya mtu mwingine ambaye wanajua kabisa alikuwa anaweza…nimegundua ma-artist wa ulaya wengine hawajafanya nanii flani labda muda mrefu lakini kwenye matukio wanahusishwa kusababisha moja ama lingine, kwa hiyo wasanii wanajiona wapo na wanaweza kufanya lolote na chochote kinawezekana. Lakini kwa sisi leo Mb Dog akitoa wimbo watu wataniita..lakini nikinyamaza kimya kesho wanakutoa kwenye hesabu, kitu ambacho kinarudisha sana nyuma muziki wa Tanzania,” Alisema Mb dog.
Mb Dog ambae hivi karibuni ameachia wimbo mpya “Ma Digina” alifunguka pia mtazamo wake kuhusu tuzo za Kili.
Msikilize hapa:
Post a Comment