Picture
                         Robert Alai


Kutoka kenya blogger  anayekabiliwa na kesi za kuchapisha taarifa za kuudhi katika mitandao Jumatano alikamatwa katika Mahakama ya Milimani Nairobi kuhojiwa na maafisa wa kuchunguza jinai.

Maafisa wa polisi waliomkamata Bw Robert Alai hawakusema sababu ya kumtia nguvuni.

Na wakati huo huo Bw Alai alishtakiwa katika Mahakama Kuu kwa kuchapisha katika mitandao taarifa za kumharibia sifa aliyewania kiti cha Ugavana kaunti ya Siaya Bw William Odhiambo Oduol.

Katika kesi iliyowasilishwa kortini na wakili Julius Otieno Juma, Bw Oduol anadai Bw Alai alichapisha habari za uwongo na kupotosha kwamba amempiga mkewe na kumjeruhi.

“Mshitakiwa amechapisha katika mtandao taarifa za kuniharibia sifa sana. Ikiwa mshitakiwa hatazuiliwa na hii mahakama ataendelea kuchapisha katika


mitandao taarifa za uwongo kunihusu,”anasema Bw Oduol katika hati alizowasilisha kortini.

Bw Oduol anaomba mahakama kuu imzuie Bw Alai kuchapisha taarifa zozote kumuhusu katika mitandao kwani “zimemfedhehesha na watu wanaziamini.”

Mwanasiasa huyo anaiomba mahakama kuu itumie uwezo wake na kumlinda dhidi ya kushambuliwa katika mitandao.

“Naendelea kuumizwa sana na habari hizo zinazosambazwa katika mitandao. Niko na hakika ni Bw Alai anayesababisha zichapishwe katika blogu zikiwa na maneno ya kunikera na kuniaibisha,” anasema mlalamishi katika kesi aliyoshtaki katika mahakama kuu.

Bw Oduol anadai kwamba mshtakiwa amefungua mitandao omundukhumundu.wordpress.com, kenyapost.com, nairobiwire.com, News4kenya.blogspot.com miongoni mwa mingine ambapo anachapisha taarifa mbali mbali.

Bw Oduol anadai mnamo Aprili 10,2013 bila idhini na akiwa na lengo la kumkejeli mshtakiwa alisababisha kuchapishwa kwa taarifa katika mtandao wa omkundukhumundu.wordpress.com

Post a Comment

 
Top