Jeshi la polisi nchini malawi
wanamshikilia kijana mmoja baada ya kumkuta akiuza sehemu ya siri ya
mwanaume.kijana huyo mwenye miaka 24 alikamatwa baada ya wananchi kutoa
ripoti kituo cha polisi kuwa kunamzee kalala relini huku akiwa anatokwa
damu nyingi ndipo polisi walipofika eneo la tukio na kumkuta mzee huyo
akiwa hio na kuamua kumkimbiza hosipitali.
Baada ya kufikishwa hosipitali ndipo
madaktari walipo gundua kuwa mzee huyo alikuwa amejeruhiwa kwa kukatwa
sehemu zake za siri,mara moja madaktari walilipoti wa maofisa hao wa
polisi na ndipo msako mkali ulipo pita katika wilaya ya Lakeshore huko
mjini Salima na polisi hao kufanikiwa kumtia mbaroni kijana huyo baada
ya kumkuta kijana huyo akiwa ktk gesti bubu akijaribu kuuza uume huo kwa
dola za kimarekani 360.
Polisi walisema mtuhumiwa Samuel
Banda alikamatwa na kiungo hicho ambacho alikuwa amekifunga ktk karatasi
nyeupe na mtuhumiwa alikiri kuwa huwa anauza viungo mbalimbali vya
binadamu kwa wafanya biashara maarufu nchini humo ambao wanaamini
wakivipata viungo hivyo huwasaidia katika biashara zao na huwaongezea
utajiri.
Mtuhumiwa Samuel Banda
Post a Comment