IDADI ya watuhumiwa wa tukio la kurusha bomu katika kanisa la
mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti Mkoani Arusha, imezidi kuongezeka
toka tisa hadi 12 kwa sasa, kati yao majina tisa yametajw ana matatu
bado ni siri kwa ajili ya uchunguzi.
Aidha jeshi la Polisi nchini kupitia Kamishana Mkuu wa jeshi
hilo,(IGP) Saidi Mwema, wametangaza donge nono la shilingi milioni 50
kwa mtu yoyote atakayefanikisha kufichua mtandao wa kigaidi nchini.
Hayo yalisemwa jana na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Arusha,
Liberatus Sabasi, wakati alipokuwa akitoa taarifa juu ya hatua
walizochukua tangua kutokea kwa mlipuko wa bomu hilo Mei 5 mwaka huu,
majira ya saa 4.300 kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,
Olasiti.
Alisema kuwa siku ya tukio kulikuwa na uzinduzi wa kanisa hilo na
mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Vatcan nchini Tanzania, Askofu Mkuu
Francisco Padilla na alipokuwa akijiandaa kukata utepe kama ishara ya
uzinduzi, ghafla mtu mmoja aliyejificha kwenye choo cha jirani, upande
wa kaskazini, alirusha kitu kizito.

Post a Comment

 
Top