Mario Balotelli ameachwa na aliyekuwa mchumba Fanny
Neguesha — siku chache baada ya kuripotiwa kusema kwamba kikosi kizima cha Real
Madrid kingeweza kulala nae ikiwa wangeitoa Borussia Dortmund.
Mwanamitindo Fanny, 22, aliondoka kwenye nyumba ya
mshambuliaji huyo huko Italia baada ya kugombana kutokana kutoelewana baina ya
wawili hao.
Straika huyo wa AC Milan Balotelli, 22, alisema wachezaji
wote wa Madrid — akiwemo Cristiano Ronaldo — wangeweza kufanya mapenzi na demu
wake Fanny ikiwa juzi wangeweza kufanya maajabu ya kugeuza matokeo ya mechi ya
kwanza (4-1) na kufanikiwa kwenda Wembley.Balo alikaririwa na gazeti la Marca
akisema: “Ikiwa Real Madrid wataenda kucheza fainali ya Champions League, nitamtoa mchumba wangu
alale nao wote.” Ingawa baadae alikana kutoa kauli hiyo.
Balotelli
aliachana na mama wa mtoto wake wa kike mtangazaji wa TV Raffaella Fico, 25, kisha ndio akaanzisha
mahusiano na mwanamitindo Fanny ambaye ana asili ya Ubelgiji.
Post a Comment