Kifo cha mwanamuziki wa Tanzania, Albert Mangwea kilichoripotiwa hivi majuzi, kinazidi kuacha maswali mengi kadiri siku zinavyozidi kusogea.
Wapo baadhi ya watu ambao wametoa maoni ya kutilia shaka maelezo na sababu za awali za kifo hicho, hali wakitumai kuwa mtu aliyekuwa naye karibu ambaye anaelezwa kuwa hai bado hospitalini, mwanamuziki M2P huenda akawa mtu muhimu wa kutoa maelezo ya kusaidia kuelewa hasa kilichotokea.
Picha ya marehemu Mangwea akiwa katika chumba cha maiti, inaonesha sura yake na shuka vikiwa vimezungukwa na utando mwekundu kama damu na hivyo kuacha shaka zaidi ya majibu endapo ni kuzidiwa kwa dawa za kulevya kulikotajwa kuwa sababu ya kifo chake, ama kuna la zaidi.
Majibu zaidi yatatoka ikiwa uchunguzi wa kina utafanyika, vinginevyo itabakia kuwa sababu halisi ya kifo cha marehemu ni siri aliyoondoka nayo. Taarifa hadi sasa zinasema kuwa mwili wa marehemu Mangwea unatarajiwa kuwasili nchini Tanzania hapo kesho, Jumamosi, Juni Mosi, 2013 kwa ndege ya South African Airways mwendo wa saa nane mchana
Post a Comment