Bus
la kampuni ya Najma linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na
Nachingwea, limepata ajali kwenye daraja la Mkapa, Ikwiriri baada ya
kugonga pikipiki na kusababisha vifo vya watu wawili papohapo.
Chanzo
cha ajali hiyo ni moshi mkali uliotanda kwenye eneo la ajali kutokana
na moto uliokuwa unaunguza majani yaliyopo pembezoni mwa barabara ya
kusini mara baada ya kumaliza daraja la Mkapa. Basi hilo lilikuwa
linatokea Nachingwea kwenda Dar es Salaam.
Watu
waliofariki ni wale waliokuwa kwenye pikipiki. Ajali hiyo imetokea
majira ya saa 6:40 mchana. Hata hivyo gari hilo halikupinduka isipokuwa
imeharibika vibaya sehemu ya mbele. Baada ya ajali hiyo, dereva
alisogeza gari kwenye kituo cha polisi cha Ikwiriri na baada ya kutoa
maelezo, polisi wameenda eneo la tukio kuchukua maiti.
Mtoa habari hii ni miongoni mwa watu waliokuwa abiria kwenye basi hilo. Namba ya gari ni T 599 CBL
Post a Comment