Chriss brown leo hii ameoneka akitemana na graffiti yake aliyokuwa
ameichora kwenye ukuta wa mbele wa nyumba yake iliyoko Hollywood, baada
ya kutakiwa kufanya hivyo, na jiji la LA baada ya majirani kulalamika
kuwa hazileti picha nzuri na zinatisha watoto wao.
Ripoti za mwanzo zilikuwa zinadai kuwa CB alikuwa anapingana na jiji la
LA tangu mwezi May kuhusu graffiti hiyo iliyokuwa imechorwa jitu la
kutisha (monster), na kupinga kuifuta kwa kudai kuwa inalindwa na 1st
Amendment ya mwaka 1792 inayodai serikali kuheshim mawazo ya aina hiyo
lakini baada ya kushindwa kwa vita hiyo Brown amesema, ameamua kufuta
kwa upendo wake yeye mwenyewe na si kwa kalazimishwa na jiji hilo au
kwa kutishiwa kulipishwa fine kubwa kw akosa hilo
Baada ya majirani kulalamika kuhusu picha hizo, jiji lilimtisha kwa
kumpiga fine kubwa kama hataifuta ----leo hii wameonekana wafanyakazi
wakipaka rangi nyingine juu ya michoro hiyo.
kwa vyovyote vile, idara ya ujenzi kitengo cha usalama cha LA imesema
kama wakaguzi wao wataridhika na ufutwaji wa graffiti hiyo, basi CB
hatapigwa fine hiyo siku ya kesho.
Post a Comment