Huu ni upande wa mbele wa fuso iliyopata hitilafu katika breki na kusababisha ajali.
Baadhi ya watu wakiwa katika eneo la ajali wakifaulisha mzigo wa ndizi katika fuso nyingine.
Haya ni mabaki ya fuso iliyogongana na basi la Metro coach maeneo ya kawawa road nje kidogo ya mji wa Moshi.
Haya ni mabaki ya ndizi yaliyotoka kwenye fuso iliyopata ajali.
Huyu ni dereva wa fuso Godluck maarufu kama Mmasi akiwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC mjini Moshi.
Huu ni mkononi wa dereva wa fuso Mmasi akiwa na pingu kwa ajili ya taratibu za kiusalama.
JANA
usiku majira ya saa moja ajali mbaya na yakusikitisha iliyotokea eneo
la barabara ya kawawa (kawawa road) iliyosababishwa na gari aina ya fuso
lenye namba za usajili T 615AWB inayomilikiwa na Dickson maarufu kama
POPA D. Kugongana na basi la Metro Coach linalofanya safari za Dar -
ArushaChanzo cha ajali hiyo ni fuso iliyokua ikitokea maeneo ya kibosho
ikiwa imebeba ndizi na maparachichi yaliyokua yakipelekwa Dar es
salaam.
Ambapo
fuso hiyo ilipofika eneo lenye mteremko hatua chache kabla ya kufika
kwenye eneo la ajali gafla dereva alijaribu kushika breki na kugundua
kua gari haina breki ndipo alipoanza kujitetea kwa kujaribu kukwepa lori
lililokua mbele yake ndio gari ikamshinda na kukutana uso kwa uso na
basi la Metro Coach. Ajali hiyo iliyopelekea dereva wa basi la Metro
Coach kupoteza maisha. Na baadhi ya majeruhi kuwahishwa katika hospitali
ya rufaa ya KCMC.
Katika
fuso kulikua na watu watatu ambao ni dereva wa fuso aliyejitambulisha
kwa jina moja la Godluck maarufu kama Mmasi, Remeni ambaye ni kondakta
na Mwenye mzigo ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa haraka.
Ambapo majeruhi wengine wamesharuhusiwa ila walipo hospitalini mpaka
sasa ni dereva wa fuso (Godluck maarufu kama Mmasi), aliyekua amekodisha
Fuso pamoja na kondakta wa Metro coach (Issa Dengu)
Post a Comment