Ni fahari na jambo la kufurahia kwa msanii yeyote afanyaye kazi na ikaubalika kiasi cha kupagawisha watu. Tunda Man amepata kujionea matunda hayo.
Msanii wa kizazi kipya - Tunda Man pichani alijikuta akishangiliwa sana na kupata wakati mgumu wa kujipenyeza popote aliposhuka kwenye gari siku ya tarehe 23.11.2013 kwenye tamasha la uzinduzi wa somo la TEHAMA mkoani Tabora katika uwanja wa Al-hassan Mwinyi, jeshi la polisi lilitakiwa kutoa msaada kwa msanii huyo kwani wanafunzi wengi wa shule za msingi waliohudhuria tamasha hilo walimzonga hali iliyotatanisha ikiwa watadondoka na kuanza kukanyagana.
[chini utaitazama video hiyo-KWA KIASI WALIHARIBU HATA UTARATIBU WA UCHUKUAJI WA VIDEO HIYO KWA SHAUKU YA KUMWONA MSANII WAO]
Akitathimini fadhira za wanafunzi kumshangilia...
wakati akiondoka na kuwaaga
Wanafunzi hawakuridhika na walizidi kulizonga gari wakati akiondoa na ilikuwa vigumu kuwazuia.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

Post a Comment

 
Top