Kiongozi wa Muslim Brotherhood Mohammed Badie
Kesi dhidi ya wafuasi 682 wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi, imeanza kusikilizwa mjini Cairo.

Watu hao ambao pia ni wafuasi wa chama kilichopigwa marufuku cha Muslim Brotherhhood, wanakabiliwa na tuhuma za kufanya maandamano yaliyozua ghasia mwaka jana.

Miongoni mwa watuhumiwa ni kiongozi wa vuguvugu hilo, Mohamed Badie.
Maafisa wa utawala wanasema kuwa Badie hatafikishwa mahakamani leo kutokana na sababu za kiusalama.
Kesi hiyo inaendeshwa bila ya watuhumiwa wengi kupo mahakamani.

Ni watu 60 pekee waliokuwa mahakamani siku ya Jumatatu ambapo zaidi ya watuhumiwa wengine miatano walihukumiwa kifo.

Wengi Nchini Misri wamelaani hukumu hiyo.
Walihukumiwa baada ya kupatikana na hatia kwa mashitaka kadhaa ikiwemo kumuua afisa wa polisi baada ya kuzuka ghasia mnamo Agosti katika makabiliano na maafisa wa usalama, wakipinga kupinduliwa kwa Mohammed Morsi.
Mawakili wao wanasema hawakuwa na nafasi ya kujitetea.
>>>>>>>>bbcswahili

Post a Comment

 
Top