Huyu aliembeba akiwa na huzuni
inayoambatana na machozi ni Moses Gift katika hospitali ya Coast
General, Mombasa ambapo picha ya Xray imeonyesha huyo mtoto bado ana
risasi kichwani.
Imefahamika kwamba risasi
iliyomuingia kichwani mtoto huyu ndiyo iliyomuua mama yake, yani baada
ya kunyooshewa silaha mama alikua ana mkinga mwanae ndio risasi ikamuua
yeye kisha ikaenda kutua kichwani kwa mwanae.
Madaktari wamekuwa wakitazama picha
za Xray na Scan kuchunguza iwapo upasuaji utafanikisha kutolewa kwa
risasi kichwani mwa Santrin bila kumpa maumivu au kuhatarisha maisha
yake.
Santrin amekuwa akilia kwa uchungu
alio nao kila wakati hospitalini huku babake akitizama tu ashindwe la
kufanya huku machozi ya kakake Moses Gift mwenye umri wa miaka 13
yakiwaleta Wakenya kwenye taswira ya unyama waliofanya magaidi wasiojali
hata watoto.
Madaktari Mombasa wamekuwa wakijadili uwezekano wa kumsafirisha Santrin hadi jiji la Nairobi kwa matibabu zaidi.
Post a Comment