Z Vile vipande vya video za Weusi zilizokuwa na title ya ‘OTEA’ ambazo zimekuwa zikiziruka kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii ya  kuanzia wiki iliyopita, tayari imefahamika kuwa ni ujio wa video ya single yao mpya ijulikana nayo kama "Gere".

Nikki wa Pili akiwa kama msemaji wa Weusi amesema kuwa wameshoot video ya ‘Gere’ Nairobi, Kenya siku chache zilizopita na director Enos Olik ambaye pia alifanya video ya nguli kuroka kule nchini kenya  Jaguar ijulikana nayo kama ‘Kioo’.

Hizi ni baadhi ya picha zao walizo achia weusi kwenye akaunti zao za kijamii





Pia niki wa pili alifunguka juu ya sababu ya wao kutofanya Video na Director Maarufu hapa bongo ajulikanaye kama Director Nisher

“Bahati mbaya Nisher alikuwa yuko caught up na mambo mengi na sisi tulikuwa na haraka so tukashindwa, kwasababu Arusha na Nairobi sio mbali tukavuka tu boda tu fasta.”

Nikki ameongeza kuwa video ya ‘Gere’ itatoka wiki ijayo.Weusi wamesema kabla video ya ‘Gere’ haijatoka wanataka kuifanyia biashara kwa yeyote anayetaka kuipata exclusive kwa siku tano kabla haijatoka rasmi iwe ni kampuni, blogs, au mtu binafsi.


“Hiyo ni biashara kwa mfano labda kampuni labda Voda au nani tunaweza tukawapa wakaweka kwenye page yao labda ya Facebook ikawa inapatikana pale tu”. aliongeza hivyo 

Post a Comment

 
Top