Raia
mmoja wa China ambaye ni mhandisi katika Kampuni ya Ujenzi ya China
Railway Bureu 15 Group inayojenga Daraja la Mto Kilombero, Qin Bao Feng
amekufa kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa ni baada ya kuboronga
katika kazi.
Ilielezwa kuwa Feng aliamua kujinyonga
baada ya nguzo za daraja alilokuwa akilisimamia katika ujenzi huo,
kusombwa na maji, jambo ambalo aliona kuwa limemvurugia kazi yake.
Baadhi ya watu waliokuwa jirani na kambi
hiyo, walisema baada ya kuharibika kwa kazi hiyo, wahandisi wenzake
kutoka China, walianza kumtenga hali iliyomfanya ajione kuwa mpweke na
hatimaye kuchukua uamuzi huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro,
Leonard Paulo alisema tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita ndani ya
kambi ya kampuni hiyo.
Alisema mwili wa marehumu ulikutwa
ukining’inia kwenye dari ndani ya chumba alichokuwa analala na kwamba
polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.
Kamanda Paulo alisema baada ya kuchunguza mwili wa marehemu walikuta karatasi iliyokuwa imeandikwa ujumbe kwa lugha ya Kichina.
Alisema kwa kuwa hakuna mkalimani aliyekuwa jirani na eneo la tukio, polisi wanaendelea kumtafuta mtu wa kuutafsiri.
Alisema kwa sasa mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya St Francis iliyopo Kilakala, Morogoro.
Chanzo;Mwananchi
Post a Comment