Wakazi wa kijiji kimoja katika wilaya ya Laikipia ya Kati nchini Kenya walipatwa na mshangao baada ya wavulana wawili kumnajisi msichana wa umri wa miaka 9, kabla ya kumuua kinyama.Kisa hicho kilitokea Jumapili alasiri katika kijiji cha Kahuruko, kata ya Lamuria, wilayani humo.Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili alikuwa akirejea nyumbani kutoka kanisani akiandamana na mamake pale wavulana wawili walipomvamia, wakamnajisi na kumuua.
“Msichana huyo alikuwa ameenda msituni kujisaidia huku mamake akiendelea na safari ya kwenda nyumbani. Alipofika nyumbani, mama alishangaa alipogundua kuwa bintiye hakuwepo na ndipo akarudi kumchukua,” Afisa Mkuu wa Polisi Tawala katia eneo hilo, Ndegwa Githinji, alisema.
Alipofika mahala pa tukio alimpata bintiye akilia kwa machungu huku akitokwa na damu mdomoni na katika sehemu zake za siri huku wavulana wawili wakiwa wamesimama kando yake.Mmoja ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya upili na mwengine aliacha shule. Wawili hao ni wanaishi boma jirani.Mwanamke huyo alipiga kamsa na wavulana hao wakatoroka. Hata hivyo, wananchi waliwakabili na kuwakamata, mmoja akiwa mtini, na wakawawasilisha kwa polisi.Wanakijiji walitaka kuwaua wavulana hao lakini polisi wakawazuia.“Msichana huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Nanyuki lakini akakata roho hata kabla ya madaktari kuanza kumhudumia.
“Walimnajisi, wakamnyonga na kumpiga na kifaa butu,” akasema Bw Githinji.
Alisema washukiwa walipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kabla ya kufungiwa katika kituo cha polisi cha Ngobit kuhojiwa.Mwili wa msichana huyo unasubiri kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Nanyuki.

Post a Comment