Stori: Musa mateja/Risasi
STAA aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’ ameibuka na kumvaa mwanadada Judith Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’ akidai amemdhalilisha kwa mashabiki wake
Akizungumza na mwanahabari wetu, Matonya alisema anamtafuta Jide popote alipo ili amuulize kinaga ubaga kwa nini aliamua kuposti picha kwenye mitandao yake ya kijamii ikimuonesha akiwa hajitambui pasipo kumtaarifu.
“Nimeumizwa sana na Jide kwa kitendo chake cha kuamua kunidhalilisha kwa kiasi hicho tena akijua mimi ni mwanamuziki mwenzake na kama kuna kitu aliona simfurahishi kwenye mwenendo wa maisha yangu basi alikuwa wazi kuniita na kunikalisha chini na siyo kama uamuzi alioutumia wa kunianika kwenye mitandao,” alisema Matonya.
Matonya alifafanua kuwa picha hiyo alipigwa katika video yake mpya lakini Jide akaichukua na kuiweka mitandaoni pasipo kumuuliza.
“Ile picha aliyoitumia kunidhalilisha ilikuwa ni ya video yangu ya wimbo mpya unaoitwa Homa ya Jiji ambayo itatoka hivi karibuni, sasa yeye ameweka mitandaoni na kusababisha watu wanidharau kwa kuona nimelewa chakari, asiponiomba radhi nitahakikisha namfikisha mahakamani,” alisema Matonya.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jide aliiposti picha ya Matonya akiwa amelala na kusindikiza na ujumbe ulioonesha kama hamjui msanii huyo hali iliyosababisha mashabiki wengi kumsema vibaya Matonya.
Related Posts
- Video; Tanesco Wagundua Wizi wa Umeme Nyumbani kwa Wema Sepetu.08 Dec 20150
Shirika la Umeme Nchini Tanesco Limekata Huduma ya Umeme Nyumbani kwa Staa kutoka kiwanda cha b...Read more »
- Tuzo Nne Walizoshinda Vanessa Mdee na Diamond Platnumz AFRIMA Hizi Hapa.16 Nov 20150
Tuzo za All Afrika Music Awards 2015 (AFRIMA) zimetolewa usiku wa Jumapili November 15 jijini Lag...Read more »
- Ulimiss Kile Kisa cha Bibi Harusi Aliyetoroka Katika Siku yako Ndoa Huko Moshi.11 Nov 20150
Bibi harusi Doroth Msuya aliyetoroka saluni akipambwa saa tatu kabla ya kufungwa kwa harusi ...Read more »
- Martin Kadinda Akieleza Juhudi Alizozifanya ili Kuomuona Jackline Cliff China Gerezani.04 Nov 20150
Jina la Jackie Cliff sio geni masikioni kwa watu kutokana na Umaarufu alikuwa nao staa huyu amb...Read more »
- Picha ya Tuzo Mpya Aliyoshinda Diamond Platnumz za MTVEAM 2015.26 Oct 20150
Msanii Diamond Platnumz Amenyakua Tuzo zingine za MTVEAM katika Kipengele cha Best World Wide...Read more »
- Baraka Da Prince yuko Mapenzini na Agness Masogange?11 Sep 20150
Hit Maker wa Single ya Nivumilie Baracka Endrew ama Baracka De Prince’ amefunguka kuwa kufu...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.