MWANAMITINDO na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo amekuwa tishio kwa msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa urembo na muonekano katika picha zinazoonekana mitandaoni nchini.
Mwanamitindo na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo.
Mtandao mmoja wa hapa nchini umeendesha zoezi la kuweka picha zao kali zinazowaonesha wote wawili wakiwa na muonekano na picha kali huku wakiuliza nani zaidi ya mwenzake.Jokate ameibuka mshindi kwa kupigiwa kura tano huku watu wakimsifia kuwa ni wa kimataifa zaidi ambapo Lulu alionekana kupigiwa kura na mtu mmoja.
Msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Amani liliongea na Jokate ambaye aliwashukuru Watanzania kwa kumpenda na kumpa nafasi lakini aliwasihi kwa kuwaambia kuwa yeye aonavyo wote ni warembo.“Mimi naona sisi wote ni warembo, nawashukuru Watanzania walionichagua na kuniona nafaa,” alisema Jokate

Lulu alipotafutwa, hakupatikana.

Post a Comment

 
Top