Tumezoea kuona wasanii mbalimbali wa Tanzania wakipata ‘endorsement deals’ za makampuni na picha zao kutumika kwenye mabango makubwa ya matangazo barabarani, kitu ambacho kwa mujibu wa Naziz ni nadra kukiona nchini Kenya.

Rapper huyo wa Kenya, Naziz amesema kuwa anaamini kuwa Tanzania ndio inaongoza kufanya vizuri kwenye sanaa ya muziki ikifuatiwa na Uganda na ya tatu ni Kenya.

Naziz ambaye yupo nchini amesema kinachosababisha sanaa ya muziki Kenya ikue taratibu ni kukosekana kwa umoja pamoja na support ya kutosha kutoka kwa makampuni.

“Nadhani nyie ndio mnaongoza kwenye hiyo sekta (muziki),” Naziz ameiambia XXL ya Clouds Fm. “Sio rahisi Kenya kwenda barabarani na kukuta msanii kwenye mabango makubwa, kwasababu corporate haisupport muziki wa Kenya, ni tofauti na hapa corporate ina support.”

“Naweza kusema Kenya tulianza vizuri sana tulikuwa miongoni mwa wale wa mwanzo Afrika mashariki kuwa na endorsements, lakini imefika sehemu kwasababu hakuna umoja…ndio sababu industry ya Kenya imestop kidogo kukua.”

Rapper huyo wa Necessary Noise ameongeza kuwa wasanii wanaochipukia Kenya wanapata ugumu kutokana na matatizo yaliyopo kwenye industry yao.

“Hatuna msanii mkubwa wa Kenya mpya ambaye ametoka ndani ya miaka sita iliyopita hamna, watu wanaoushikilia muziki ni wale wale waliokuwepo.”

Post a Comment

 
Top