Kuna barua iliyosambaa mtandaoni weekend hii inayoonekana imetoka kwenye mamlaka ya mapato nchini, TRA ikiutaka uongozi/kampuni inayosimamia kazi zake kuwasilisha nakala za mkataba wa makubaliano kati yao kuhusiana na masuala ya promotion katika kipindi cha kuanzika mwaka 2010 – 2014.
Barua hiyo pia inaongeza kuwa:"Unatakiwa pia kuwasiliasha vielelezo vya ushahidi kuhusiana na huduma iliyofanyika na kiasi cha fedha kilicholipwa kulingana na ajira ya Abdulmalik Naseeb.”
Hata hivyo uongozi wa Diamond umedai kuwa barua hiyo nao wameiona kupitia mtandaoni lakini haijawafikia mkononi.
“Tunasikia tu kwenye mitandao hatuna taarifa nayo, maana hawajawasiliana na sisi,” amesema Salam, mmoja wa mameneja wa Diamond Platnumz.
“Inashangaza kuona kitu kwenye mitandao bila ya kuambiwa mhusika mkuu, tumechukulia kama changamoto zilizopo kwenye maisha,” ameongeza.
Diamond bado yupo nchini Nigeria alikoenda kutumbuiza kwenye ‘The Africa Magic Viewers’ Choice Awards 2015’.
Post a Comment