Kutoka kwenye Gazeti la Habari leo wametoa taarifa kuhusu mmiliki wa cha kipya ambacho aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini amehamia uko baada ya kusitishwa na chama cha Chadema kwa madai ya kuwa ni msaliti na limeandika kama ifuatavyo
CHAMA cha Mabadiliko na Uwazi (ACT), kimetangaza rasmi kuwa muasisi wa chama hicho ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), ambaye kwa sasa bado anatambulika kuwa mwanachama wa Chadema.
Siri hiyo iliwekwa hadharani jana na Makamu Mwenyekiti wa ACT, Shabani Mambo, wakati akinadi kwa wananchi wagombea wa uenyeviti wa serikali za mitaa kupitia chama hicho kipya, katika mitaa ya Majengo pamoja na Nyasubi katika uwanja wa Lumambo.
Kutokana na kauli hiyo, gazeti hili lilimtafuta Zitto atoe ufafanuzi, ambapo alikataa kukiri wala kukanusha madai hayo ya ACT.
Hii si mara ya kwanza kwa Zitto kuhusishwa na chama hicho, ambapo Mei mwaka huu alipohojiwa na kituo cha redio cha Clouds Fm, kiongozi huyo kijana wa Chadema alikaririwa akisema hawezi kukubali au kukanusha kuwa mwanachama wa ACT, mpaka hapo kesi ya msingi dhidi ya uanachama wake Chadema itakapotolewa uamuzi mahakamani.
Aliulizwa swali hilo, baada ya kiongozi ambaye alitimuliwa Chadema pamoja na Zitto, Profesa Kitila Mkumbo, kumtaka rafiki yake Zitto kuhamia ACT na kugombea nafasi ya uenyekiti.
Profesa Mkumbo katika maoni yake kwa Zitto, alikaririwa akisema kiongozi huyo kijana hawezi kupata mafanikio zaidi ya kisiasa ndani ya Chadema, isipokuwa kama ataamua kuhama chama hicho.
Zitto alipohojiwa na Clouds kuhusu kauli ya Profesa Mkumbo, alisema yeye na Profesa Mkumbo wana mrengo wa siasa unaofanana, unaoamini katika maendeleo na maslahi ya jamii kwa ujumla na sio chama wala watu wachache.
Kampeni
Akiendelea na kampeni baada ya kueleza kuwa bosi wao ni Zitto, Mambo alidai watumishi wa Serikali iliyopo madarakani, wamekuwa na jeuri ya fedha kuliko wafanyabiashara hata kama wana mishahara midogo na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana na ubadhirifu uliopo katika sehemu zao za kazi.
“Unakuta mfanyakazi mdogo wa halmashauri lakini unakuta anamiliki mali nyingi na huku mshahara wake ukiwa ni mdogo, ukiambiwa unaweza kushangaa hata mfanyabiashara mkubwa anaweza kutokuwa nazo sasa hebu fikiri mtu huyu anatoa wapi fedha hizo?” Alihoji.
Katika Mkutano huo Makamu Mwenyekiti huyo aliwanadi wagombea uenyekiti kupitia ACT kutoka katika ya Majengo Kati, Ali Shango pamoja na mgombea mwingine wa Mtaa wa Nyasubi, Idsam Mapande na kuongeza kuwa chama hicho ambacho ni kipya kimejipanga kuhakikisha kuwa kinashinda viti hivyo.
Related Posts
- Chama Cha Mawakala wa Forodha Nchini Chaibua Mapya Kuhusu Utoroshwaji wa Makontena15 Dec 20150
CHAMA cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA) kimesema kuwa wizi wa kontena bandari ya Dar es ...Read more »
- David Kafulia Kunguruma Mahakama Kuu Kupinga Ushindi wa CCM Jimbo la Kigoma Kusini.17 Nov 20150
Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR -Mageuzi, David Kaful...Read more »
- CCM Yazoa Viti Maalum Vya Udiwani 1021 Huku Wapizani Wachukua Viti 371 Tu.14 Nov 20150
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imetangaza idadi ya viti maalum kwa nafasi ya udiwani ...Read more »
- Picha za Maalim Seif Pamoja na Viongozi wa Ukawa Wakizungumza na Balozi wa EU na Kutoa Msimamo Mzito.14 Nov 20150
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amerejea kauli yake ya k...Read more »
- Nape Nnauye Aelezea Sababu za Jina la Irene Uwoya Kukatwa kwenye Ubunge wa Viti Maalum.10 Nov 20150
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Nape Nnauye amefunguka suala la msanii wa Bong...Read more »
- Wagomba Zanzibar Waandika Barua Umoja wa Mataifa UN.04 Nov 20150
Wagombea wa urais wa Zanzibar wa vyama sita, wamemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mata...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.