Taarifa zilizo nifikia hivi punde zinasema kuwa Wanachama Saba (7) wa Klabu ya mpira ya Jijini Dar es salaam Simba Sports Club maarufu kama Simba UKAWA wamefariki dunia baada ya kupata ajali ya basi jana Aprili 3, mkoani Morogoro.


WANACHAMA 7 WA SIMBA SC WAFARIKI KWA AJALI


Ajali hiyo imetokea mapema leo maeneo ya Mkundi nje kidogo ya manispaa ya Morogoro chanzo cha ajali hilo ni gari lao kukosa balance na kupinduka baada ya kupishana na gari lingine na kupoteza muelekeo.


WANACHAMA 7 WA SIMBA SC WAFARIKI KWA AJALI


Watu 5 waliaga Dunia palepale na wawili waliokuwa majeruhi kufariki katika hospitali ya mkoa wa Mororgoro walipokuwa wakipewa matibabu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Leonard Paul amethibitisha habari hizi na kusema kuwa majeruhi wamebaki 13 na kufanya vifo kufikia saba hadi majira ya saa 2 usiku wa April 03.


Post a Comment

 
Top