Ile Story ya Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima bado inaendelea na kwa sasa nakuletea baadhi ya mali anazomiliki na taarifa zake nyingine ambazo huzijui kabisa.
Kipindi cha nyuma niliwah kukuletea taarifa za Mchungaji Gwajima kufikishwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maaalum ya Dar es Salaam baada ya kumtusi Askofu wa Kanisa la Romani Katoliki Jimbo Kuu la Dar, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo ambapo alikimbizwa hospital baada ya kuzidiwa kwa hofu na uoga.
Hii ni picha ya Mali anazomiliki mpaka sasa
Anamiliki gari aina ya Hammer ambayo kwa mahesabu ya haraka haraka ni kiasi cha million 250 za kitanzania.Pia mchungaji Gwajima amewanunulia wachungaji wake 30 magari ya kutembelea ili kupambana na tatizo la usafiri jijini Dar.Magari mengine anayomiliki ni pamoja na Subaru Forester (sokoni linauzwa shilingi milioni 17), Mitsubishi Pajero (shilingi milioni 16), Toyota Spacio new model (milioni 20) na Toyota Harrier Lexus (milioni 35).
Nyumba ya kifahari ya ghorofa nne iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Gwajima alinunua helkopta (chopa) kwa ajili ya kuzungukia sehemu mbalimbali nchini kutoa huduma ya kiroho. Uzinduzi wa helkopta hiyo ulifanywa na mbunge wa Monduli (CCM) na waziri mkuu wa zamani, mheshimiwa Edward Lowassa.
Anamiliki mabasi 20 ambayo ni kwa ajili ya kuwabeba waumini wa kanisa lake wakati wa kwenda kwenye ibada na kurudi makwao katika sehemu mbalimbali za Jiji la Dar. Mabasi hayo kila moja alilinunua kwa shilingi milioni mia moja na ishirini.
Kanisa la Mchungaji Gwajima linaongoza kwa kuwa na waumini wengi ambapo wanakadiriwa kufikia 70, 000. Kwa maana hiyo sasa, kama waumini wake watatoa sadaka ya Jumapili kila mmoja kwa shilingi elfu mbili, atakuwa anaingiza shilingi milioni 140 kwa ibada moja.Kwa mwezi, Gwajima atakuwa anaingiza shilingi milioni 560 japokuwa wapo waumini inadaiwa hutoa hadi shilingi laki tano (500,000) kama sadaka kwa ibada moja.
Credit GPL
Post a Comment