Ukatili aliyofanyiwa Hanafi Daudi (31) ambaye ni mkazi wa Salasala Kilimahewa jijini Dar es Salaam, yupo katika hali mabaya baada ya kwagiwa mafuta ya moto yalikuwa jikoni yakikaangia chipsi alifanyiwa kitendo hicho baada ya kwenda kukopa chipsi kwa muuzaji wa kibanda hicho.

Mwanaume Aliyechomwa na Mafuta ya Moto

Akifanya mahojiano na Global Publisher alikuwa na haya ya kusema 

“Ilikuwa usiku wa saa 3:30 hivi, muda ambao watu walikuwa wanaangalia mpira. Ndipo nilipoamua kwenda pale kwa lengo la kuomba kukopeshwa chipsi kwa kuwa sikuwa na pesa muda huo. Niliamini ningemlipa kesho yake"

Mwanaume Aliyechomwa na Mafuta ya Moto

“Nilipofika, yule jamaa nilimuona kama yuko tofauti hivi lakini nikaamua nimuombe anisaidie kwa muda ule. Nikashangaa tu akanyanyua karai la mafuta ya chipsi na kunimwagia usoni.Nilihisi kuchanganyikiwa, nikakimbia mpaka kwa wenzangu. Wakati huo macho yote yalikuwa yameziba, sioni kitu chochote. Ndipo wenzangu wakanibeba na kunileta hapa Muhimbili kwa msaada wa usafiri njiani,” 

Mwanaume Aliyechomwa na Mafuta ya Moto

“Wale wenzangu baada ya kunifikisha hapa na kuondoka sijawaona tena mpaka leo. Sina msaada wowote, sina ndugu wa kunisaidia, sina mawasiliano na watu wa nyumbani Tanga.
“Najisikia vibaya sana kwa sababu mtuhumiwa alikimbia muda uleule aliponifanyia ukatili huu. Kikubwa ninamwomba Mungu anisaidie kwani yeye ndiye anayejua cha kunifanyia.”

Mwanaume Aliyechomwa na Mafuta ya Moto

Post a Comment

 
Top