WALIOKOSA NAFASI KIDATO CHA TANO WACHAGULIWA UALIMU UDOM,ANGALIA MAJINA HAPA


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wamefanya uchaguzi wa wanafunzi kwenye mafunzo ya Ualimu kwa kozi za Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Msingi na Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Sekondari Sayansi na Hisabati ambayo yataendeshwa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma. Uchaguzi huu ni kwa wale wahitimu wa kidato cha nne kwa mwaka 2014 waliofaulu kwa daraja la Krediti na zaidi lakini hawakupangiwa kidato cha tano. Utaratibu wa kuripoti utatolewa na chuo husika punde watakapomaliza maandalizi ya kupokea wanafunzi hawa. Majina ya waliochaguliwa kujiunga na masomo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 yameambatinishwa HAPA au Download hapa.


Post a Comment

 
Top