Kajala na Wema wakipozi pamoja.


Mastaa wawili kutoka Kiwanda cha utengenezaji wa Filamu Hapa BongoMovie Staa Wema Sepetu pamoja na Kajala Masanja ambao wamekuwepo kwenye Ugomvi mkubwa kisa kikidaiwa ni matusi ya hadharani na kuzalishana kwa warembo hawa.

Kajala amekuwa amkijaribu kuomba msamaha kupitia njia Tofauti tofauti lakini imekuwa haimuingii akilini kabisa shosti wake Wema Sepetu lakini mapema week Wema aliamua kuvunja ukimya na kutaka kumaliza tofauti iliyopo baina yake na Kajala na haya ndio aliyosema

“Kiukweli kabisa nimeshamsamehe Kajala, sina tatizo naye, hivyo muda wowote akinihitaji kwa lolote sina kinyongo kabisa.Nimefikiria kwa kina, nikaona sina sababu ya kuendelea kuwa na chuki naye na kupitia hilo namuomba Mungu aendelee kuniongoza ili nifute kabisa hilo wazo la chuki moyoni.Nipo radhi kukutana naye mahali popote pale endapo atanihitaji au mimi nitakapomuhitaji nitamtafuta,” 


“Najua itakuwa ngumu sana kwa watu kuniamini kwa sababu hapo nyuma kulikuwa na mambo mengi kati yetu, naendelea kuwatoa wasiwasi kwa kuwaambia tena kuwa tayari moyo wangu umeshamsamehe Kajala na nimejishusha kwa kila hali kwake.Nipo radhi kukutana naye mahali popote tukaongee ili wale wanaohisi sijamsamehe waamini hilo.”


Kajala naye alikuwa na haya ya Kusema


“Kwanza nashukuru kusikia hivyo, binafsi sina tatizo na hilo, kikubwa namshukuru maana nimekuwa nikimuomba Wema kupitia sehemu mbalimbali ili tumalize tofauti zetu lakini alikuwa akikataa, ila kama mwenyewe anasema yupo tayari tuyamalize, kwangu ni furaha.Nimekuwa nikipigania hilo kila kukicha, sasa naamini Mungu atakuwa amesikia kilio changu kwa mara nyingine, napenda kusema sina tatizo lolote katika hilo,” alisema Kajala.


Wema Sepetu ambaye kwa sasa anagombea Ubunge kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Singida Jimbo la Singida Mjini amechukua Fomu tayari na kinachosubiriwa ni kampeni tu kuanza mapema iwezekanavyo..

Source GPL 

Post a Comment

 
Top