Lowasa ashindwa kwenda kumzika Kisumo, msafara wake wazuiliwa na polisi.

Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama cha Chadema Mh Edward Lowassa Mapema leo alizuliwa kufika msibani na polisi mkoani Kilimanjaro alipokuwa akienda kuhudhuria maziko ya aliyekuwa mwanasiasa mkongwe mzee Peter Kisumo alikuwa anazikwa Usangi Mkoani Kilimanjaro. Mh Lowassa ambaye aliwakuwa ameambatana na wafuasi wa chama hicho walizuliwa na polisi.Hii ni taarifa toka ITV 

Gari la Mh Lowassa ambaye pia ni mgombea urais wa Chadema akiwakilisha Ukawa lilianza kufuatwa na magari mengine ya watu binafsi na pikipiki baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro akitokea na Dar es Salaam na alipofika Moshi kundi la vijana walifunga barabara na kulazimika kuingia katika hotel ya kizi ambako pia walimfuata na kuzingira lango kuu na licha ya kuwasihi kuwa wampe nafasi aende kwenye mazishi vijana hao waliendelea kulifuata gara lake. 

Katika hali ambayo sio rahisi kuamini vijana hao wakiwa na pikipiki waliendelea kufuata gari la Mh Lowassa hadi Mwanga na alipoanza safari ya kuelekea Usangi takrbani kilometa moja kutoka barabara kuu polisi wakafunga barabara hali iliyosababisha mvutano mkubwa na jambo ambalo limelalamikiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya viongozi akiwemo mwenyekiti wa NCCR mageuzi James Mbatia na Mh Agustino Mrema.

Baada ya vuta nikuvute kati ya polisi na wananchi na viongozi hao wa vyama vya siasa mkuu wa polisi wa wilaya ya Mwanga aliruhusu watu waliokuwa na pikipiki kuendelea na safari kwa masharti ya kuondoa bendera za vyama vyao na pia kwenda bila msafara maelekezo ambayo licha ya kubalika utekelezaji wake ulikuwa mgumu na kusababisha kuendelea kwa malumbano na ndipo Mh Mbatia akata taarifa za Mh Lowassa kusitisha safari na kuamua kurudi Moshi na hatimaye Dar es Salaam.




Lowasa ashindwa kwenda kumzika Kisumo, msafara wake wazuiliwa na polisi.


Lowasa ashindwa kwenda kumzika Kisumo, msafara wake wazuiliwa na polisi.


Lowasa ashindwa kwenda kumzika Kisumo, msafara wake wazuiliwa na polisi.


Lowasa ashindwa kwenda kumzika Kisumo, msafara wake wazuiliwa na polisi.

Post a Comment

 
Top