Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imetangaza idadi ya viti maalum kwa nafasi ya udiwani kwa kila chama.

Chini ya mgawo huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeongoza kwa kupata viti 1,021 na upinzani 371.


Kwa mgawanyo huo, jumla ya madiwani wa viti maalum nchini ni 1,392 ambapo viti 14 vilivyosalia, vitajulikana baada kufanyika uchaguzi wa marudio katika kata 34 ambazo hazikufanya uchaguzi kutokana na kasoro mbalimbali na vifo kwa baadhi ya wagombea.


Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, imeonyesha kuwa kata 3,975, ndizo zilifanya uchaguzi mkuu mwaka huu.


“Kwa mujibu wa Sheria Nec imepewa mamlaka ya kushughulikia na kutangaza Viti Maalum vya Madiwani Wanawake visivyopungua 1/3 ya madiwani wa kuchaguliwa katika kila halmashauri ambayo 1/3 ya 3,975 ni viti 1,406,” alifafanua. Jaji Lubuva alitaja kwa kila chama na idadi ya madiwani waliopata kwenye mabano kuwa ni CCM (1,021), Chadema (280), CUF (79), ACT- Wazalendo (6) na NCCR Mageuzi (6).


Alibainisha kuwa majina ya madiwani hao yatapatikana kwenye vyama na halmashauri husika na kwamba uteuzi huo umezingatia orodha iliyowasilishwa Nec na vyama husika.


“Novemba 14, mwaka huu, Nec itatangaza majina ya majina ya madiwani wa viti maalum walioteuliwa,” alisema.

Post a Comment

 
Top