Alphonce Mawazo

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, jana lililazimka kupiga mabomu ya macho katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), kuwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wameupokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo aliyeuawa kwa kukatwa mapanga.


Tukio hilo lilitokeaza jana jioni, baada ya wafuasi hao kuanza mvutano na askari Polisi mmoja na ndipo zikaibuka vurugu zilizodumu kwa saa moja na nusu.


Hata hivyo wafuasi hao kabla ya kuanza vurugu hizo, waliruka kuta za hospitali na kufungua geti kwa mabavu.


Mwandishi alishuhudia Polisi huyo na wafuasi wa Chadema wakivutana nje ya mlango wa vyumba vya kuhifadhi maiti.


Baada ya mvutano huo wafuasi hao wa Chadema walianza kumuangushia kichapo askari huyo ambaye anatuhumiwa kufanya njama za kurudisha mwili wa marehemu mkoani Geita kwa madai kwamba tukio lilitokea huko.


Hali hiyo ya askari kuangushiwa kichapo, ilisababisha gari la polisi ambalo lilikuwa na polisi ambao walikuwa na mabomu ya machozi na silaha za moto kuanza kupiga mabomu.


Aidha Mwandishi wa habari hizi, alishuhudia Polisi mmoja akimpiga mjane wa marehemu, katika vurugu hizo ambazo wafuasi wa Chadema walikuwa hawataki polisi waingie ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti.


Katika vurugu hizo, polisi walimtia mbaroni Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Pastrobas Katambi na baadhi ya wafuasi zaidi ya wanne.


Awali wakati wafuasi wa Chadema wakiupokea mwili wa marehemu, walikuwa walisikika wakiimba, “Kama sio wewe Mkapa na mauaji yangetoka wapi.”


Wafuasi hao waliupokea mwili wa marehemu katika kivuko cha Busisi ambapo walipofika kati kati ya Jiji la mwanza walitokea wafuasi wengine ambao walikuwa nao walisikika wakiimba,” CCM wameua CCM wameua…" hadi katika BMC.


Kifo cha Mawazo kinahusishwa na tofauti za kisiasa kati ya chama cha Mapinduzi(CCM) na Chadema..


Mawazo ambaye alikuwa ni mgombea ubunge jimbo la Busanda akichukuana na Lolencia Bukwimba (CCM) inadaiwa alikuwa anatarajiwa kwenda mahakamani kupinga ushindi wa Bukwimba.


Hata hivyo inaelezwa kuwa endapo marehemu angefungua mashtaka polisi huenda angeshinda kesi hiyo kutokana na ushahidi wa video alizodai kuwa nazo zikiwaonesha polisi wakiwatisha mawakala wa Chadema kusaini matokeo kwa lazima.


Akizungumza na wafuasi wa Chadema, Godbless Lema, alisema kifo cha Mawazo ni mpango wa Chama cha Mapinduzi na kuitaka Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaohusishwa na kifo hicho.

Post a Comment

 
Top