Muigizaji amabe anafanya vizuri sana kwenye tasna ya bongo movie pia mmiliki wa kampuni ya Endless film Wema Sepetu baada ya kumpa kajala shavu la kufanya kazi ndani ya kampuni yake amesema yeye kama Wema sepetu hategemei Kajala kujakufanya kazi katika kampuni ili kumlipa zile million kumi na tatu 13 alizomsaidia ili asiingie jela


Wema sepetu aliongea kwenye kipindi cha XXL, Wema amesema Kajala atakuwa akifanya kazi zake lakini atakuwa akimlipa kama kawaida. Ambapo Kajala kwa sasa atacheza filamu moja inaitwa Princess Sasha ambayo atacheza kama mhusika mkuu  kwenye filamu hiyo.

“Tutaenda kuishoot nje ya Dar, ninataka kuishoot mandhari fulani hivi kama ya kijijini. Ni mtoto wa mfalme, Kajala ndo atakuwa Princess Sasha, she is going to be the main character, “ alisema Wema.


Kajala naye amesema aliamua kujichora tattoo ya jina la Wema kwasababu anamchukulia kama shujaa.

“Mi naweza kusema nimeichora kuonesha nimeappreciate vipi kitu alichonifanyia , watu wengine wanaichukulia vibaya, wataongea vibaya, lakini mimi najua moyoni mwangu. Sababu nimeona siwezi kumlipa hiyo hela sasa hivi.

Ntamkumbuka siku zote hata chochote kikitokea atabakia kuwa mtu… yaani she is my hero.”

Post a Comment

 
Top