Muigizaji mwenye sauti ya
kiume katika filamu za
Kibongo, Yusuf Mlela
ameiminyia mavumbini
skendo inayomtafuna
kwamba anatoka kimapenzi na msanii mwenzake, Aunt
Ezekiel Grayson.
Akizungumza hivi karibuni
jijini Dar, Mlela alisema kuwa,
anawashangaa wazushi
wanaoneza madai hayo lakini akasema anajua ni kutokana
na jinsi wanavyogandana na
msanii huyo kama
kumbikumbi maeneo
mbalimbali.
Aliongeza kuwa, licha ya kwamba Aunt ni msanii
mwenzake lakini pia
wameshibana ile mbaya,
akaomba watu wasiwatafsiri
vinginevyo.
“Unajua mimi na Aunt wote tunaishi kwa kutegemea
sanaa, hicho ndiyo kitu
kinachotufanya tuwe karibu,
zaidi ya yote huwa tunakuwa
kampani moja tunapokwenda
disko au kwenye sherehe mbalimbali, ila kila mmoja ana
mtu wake,” alisema Mlela. Alipobanwa kuhusu
kualikwa kwenye
mashindano ya Miss Tanzania
2011 na kadi yao kuonekana
kama ya Mr & Mrs huku
wakiingia ukumbini hapo kama wanandoa, Mlela
alijitetea:
“Watu wanaotualika kwenye
sherehe zao ndiyo walitupa
kadi moja. Hata siku ile ya
Miss Tanzania tulipewa kadi ya mwaliko moja tu ikiwa na
majina yetu, ndiyo maana
ulituona vile.”
Mbali na Miss Tanzania 2011,
katika harusi ya msanii
mwenzao, Irene Uwoya iliyofungwa jijini Dar es
Salaam mwaka 2009, wawili
hao pia walikuwa beneti hali
iliyoibua maswali kibao
kwamba huwenda wawili
hao ‘wanaduu’.Muigizaji mwenye sauti ya

hao ‘wanaduu’.

Post a Comment

Top