Mwigizaji mwenye mvuto
kwenye kila idara
anayejulikana kama Rose wa
Ndauka hivi karibuni
amefunguka kuhusu utata
uliokuwepo kati yake yeye na Wema wa Sepetu
uliotokana na kuvunjika kwa
moja ya kundi la filamu
walilokuwa wameliunda
kipindi kifupi
kilichopita.Kundi hilo lililokuwa likiundwa na
Wema,Rose na jackline
lilikuwa likijulikana kama
JAROWE likimaanisha majina
matatu ya warembo hao.kwa
kila jina kuchukuliwa herufi yake ya kwanza.Kundi hilo
lilifanikiwa kutoa filamu moja lakini muda
mfupi baadae likavunjika na
kuibua uhasama baina ya
warembo hao,huku kila
mmoja akidai kuibiwa maslai
ya filamu waliyoitoa.Lakini mda mchache uliopita Rose
aliibuka na kusema kuwa
yeye hana tena bifu na wema
kutokana na mgogoro
uliotokea na kueleza kuwa
japo kwa sasa wanaongea japo si kwa ukaribu sana
kama zamani,yeye hana
kinyongo naye na yuko
tayari kama wataitwa
wacheze filamu moja.,ni hayo
kutoka kwa Ndauka.

Post a Comment

 
Top