WIKI hii Ten Questions
inagonga mlangoni kwa
msanii ambaye anafanya
vizuri katika anga la muziki
wa Bongo Fleva. Anaitwa
Khaleed Ramadhan ‘2nda Man’ aliyezaliwa
Agosti 18, 1987 katika
Hospitali ya Ocean Road jijini
Dar es Salaam.
Alianza kufuta ujinga mwaka
1994 katika Shule ya Msingi Makurumla, Magomeni jijini
Dar es Salaam na baadaye
aliendelea kupiga buku katika
Shule ya Sekondari Forodhan.
A-Level alisoma Sekondari ya
Makongo, zote zipo Bongo. Hayo ni kwa ufupi tu lakini
mengi zaidi ungana nami
kwenye maswali kumi hapa
chini.
TQ: Muziki ulianza lini na
wimbo wako wa kwanza uliitwaje?
2nda: Nilianza mwaka 2006 na
wimbo niliotoka nao
unakwenda kwa jina la Neila.
TQ: Hadi sasa ni mafanikio gani
ambayo unaweza kujivunia kutokana na kazi zako za
muziki?
2nda: Mafanikio binafsi ni
mengi ila kubwa zaidi ni
kwanba nikifa nitazikwa na
watu wengi sana. TQ: Ni ugumu gani
uliokumbana nao wakati
unaanza kazi ya muziki?
2nda: Katika kurekodi, maana
sikuwa na fedha za kutosha
hivyo ilinichukua muda kujipanga, sasa namshukuru
Mungu kwa hapa nilipo.
TQ: Vipi kuhusu matumizi ya
siku, unatumia shilingi ngapi?
2nda: Chakula hunichukulia
fedha nyinga sana, kwani sijui kupika kabisa hivyo ni lazima
nile hotelini. Nateketeza si
chini ya elfu thelathini kwa
siku.
TQ: Sasa tuingie kwenye
maisha yako ya kimapenzi, vipi una mpenzi?
2nda: Ndiyo tena nampenda
sana.
TQ: Vipi usumbufu kutoka
kwa mademu micharuko?
2nda: Usumbufu ni mkubwa sana lakini najua jinsi ya
kukabiliana nao.
TQ: Ukiwa katika shoo za
mikoani hupati vishawishi
vya kumsaliti mpenzi wako?
2nda: Mara nyingi huwa naambatana na mpenzi
wangu kwa hiyo ni vigumu
kumsaliti.
TQ: Ukiwa chumbani na
mpenzi wako ni jambo gani
linakufurahisha zaidi? 2nda: (Huku akicheka). Mpenzi
wangu hupendelea kuvaa

Post a Comment

 
Top