Unapaswa kukubali kuachia
vipaumbele vyako ili umpe
nafasi mwenzi wako. Ni mchezo mdogo lakini
mgumu, maana yake ni
kuyaweza mapenzi. Ni jambo
ambalo lipo karibu na
kutowezekana kwa mpenzi
wa mpira kuacha ‘rimoti’ ya televisheni kwa mwenzi
wake ili aangalie tamthiliya. Hata hivyo, endapo
mtagombea rimoti, mwisho
mtaanza kuchokana mapema. KUNA MABADILIKO?
Ni vema kujiuliza swali hilo na
matawi yake. Hii itakusaidia kutanzua
mambo ambayo yanaweza
kusababisha uhusiano wenu
ukaenda na maji hapo
baadaye. * Kuna kiasi cha mabadiliko
kwa kila mmoja wenu tangu
mlipokutana kwa mara ya
kwanza?
* Bado unachangia na mwenzi
wako kila kitu chenu kama ambavyo mlifanya wakati
mnaanza kupendana?
* Kinatokea nini pale kila
mmoja anapofanya mambo
anayojisikia mwenyewe?
* Una muda kiasi gani kuwa pamoja na mwenzi wako? Je,
unajihisi upo kwenye
uhusiano imara na
wenyemafanikio? Jiulize,
inamaanisha nini kuwa na
maslahi tofauti kati yako na mwenzi wako?
* Umewahi kutafakari na
kugundua kwamba wewe na
mwenzi wako, kila mmoja ni
mtu huru lakini mmeamua
kuwa pamoja au zipo dalili za kifungo?
* Je, unaamini mapenzi ni
kujitoa mhanga? Kama
ndivyo ni kwa nini? JADILI MASWALI HAYO NA
MWENZIO
Lazima maswali hayo
uyapatie majibu, si kwa
wewe peke yako bali kwa
kushirikiana na mwenzi wako. Kama kuna sehemu yenye
utata basi haraka sana itoleeni
macho na kuondoa tofauti.
Hakikisha kila kitu kinakuwa
chanya. Hata hivyo, pengine kila
unapoweka mezani ‘ishu’ ya
kujadili inageuka ubishi. Ndani
ya ubongo wako, unaamua
kuachana na ‘topiki’ hiyo
kwa lengo la kuepuka migogoro. Unahisi mbele ya ubishi kuna
ugomvi, nawe hupendi
kugombana kwani inaweza
kuhatarisha mapenzi yenu. Hata hivyo, kuacha kujadili
jambo ambalo
linawatofautisha ni hatari
zaidi, hivyo ni busara
kutafuta meza ya
mazungumzo kwa namna yoyote ile. Ni kosa kubwa kuwa na
maslahi tofauti kwenye
mapenzi. Mnaweza
kutofautiana mambo mengine
lakini siyo hilo. Mathalan, wewe unaamini
kwamba mpenzi uliyenaye
kwake ndiyo umefika, yeye
hilo halipo akilini. Unawaza ndoa mwenzako
anakutafsiri kama ni wa
kuzugia. Uhusiano wa namna hiyo
haupo sawa, una matege,
haufai kuendelea kujengwa.
Unaweza kumrekebisha,
kama habadiliki, ni bora
ukimbie. Ni vema ukajiuliza
mwenyewe, ni kwa muda
gani utaishi na mtu ambaye
hana mpango na wewe? Kila
ukianzisha mada ya ndoa
anakuwa mkali. Lazima wote muwe na
maslahi ya aina moja, nyote
mtamani kuoana, hapo
mtaweza kufika, vinginevyo
utakuwa unajenga,
mwenzako anabomoa. Kama nilivyotaka ujiulize
hapo juu, kwamba wewe na
mwenzi wako kila mmoja ni
mtu huru. Hii inamaanisha
kuwa mapenzi siyo kifungo. Unapaswa kumuacha aamue
mwenyewe kuhusu hatma ya
mapenzi yenu. Ukionekana unambana,
anaweza kufanya mambo
kukuridhisha lakini kuna siku
atakuadhiri. Baadaye anaweza kuthubutu
kukwambia: “Sikutaka
kufunga ndoa na wewe, sema
tu ulinilazimisha.” Kauli hii ni
tusi, endapo utaitafakari kwa
mrengo kuwa uliyenaye hana mapenzi ya dhati nawe. Hata kuwa naye ni kama
umemlazimisha. Tafakari kisha upate jibu
kwamba mwenzi wako hana
hisia na wewe. Huo ndiyo
ukweli kwa maana mapenzi
ni hisia. Kama mwenzi wako
anakupenda, maana yake ana
hisia juu yako, baada ya hapo
sasa tafsiri kinyume chake.
Unaweza kujiona mdogo
kama piritoni.

Post a Comment

 
Top