WEMA Isaac Sepetu,
mwenye kibendi cha miezi
miwili kasoro alichopachikwa
na ‘kidume’ Naseeb Abdul
Jumaa ‘Diamond’, amegeuka
kero kwa baadhi ya mastaa Bongo hasa wa kike
kutokana na kutema mate
ovyo, kujichetua na kuinadi
mimba yake kupita maelezo. Akizungumza na The Biggest
IQ Paper, Ijumaa Wikienda
ndani ya Viwanja vya Leaders
Club, Kinondoni jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki
iliyopita, Wema alisema kuwa kinachosababisha awe kero ni
dalili za wazi za mjamzito
alizonazo ikiwemo kutema
mate ovyo, kubagua vyakula
na kudeka kupitiliza. Alifunguka: “Wanasema
nawakera, lakini nahisi
wananionea gere na mimba
yangu. Mimi sina chuki na mtu
yeyote na naomba
wanivumilie.”

Post a Comment

 
Top