JAMAA anayejitambulisha
kwa jina la Kuku Mtamu
kwenye Mtandao wa Kijamii
wa Facebook, amemtongoza
Naibu Katibu Mkuu wa Chama
cha Wananchi (Cuf), Julius Mtatiro.
Uwazi limefanikiwa kuyanasa
mazungumzo ya Kuku Mtamu
na Mtatiro kwenye ukurasa
wa Kuku Mtamu.
Imebainika kuwa Kuku Mtamu alimtumia ujumbe
Mtatiro kuwa anampenda
kabla mheshimiwa huyo
aliyegombea ubunge Jimbo la
Igunga, kujibu kwenye ukuta
‘wall’ wa shoga huyo: “Ha ha haaaaa, unampenda
mwanaume mwenzio? duh,
sasa kweli kazi.”
Kuku Mtamu aliipenda kauli
hiyo na kubonyeza kitufe cha
‘like’ kisha akachangia: “Serious bro, nakupenda
tenasaana.” Hata hivyo,
Mtatiro hakujibu tena na
kuwaacha wachangiaji
wengine wakimshambulia
Kuku Mtamu.

Post a Comment

 
Top