MSANII asiyechuja katika
Tasnia ya Filamu Bongo,
Christina Manongi a.k.a Sintah
‘J Lo wa Tz’ amemvaa dogo
anayekimbiza katika ‘game’
la muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na
kumpa ‘makavu’ kwa
kitendo cha kumpiga chini
mpenzi wake, Wema Isaac
Sepetu, Risasi Mchanganyiko
linaandika kifua mbele. Akizungumza na mwandishi
wa habari hizi katika
mahojiano maalum
yaliyofanyika juzi, jijini Dar es
Salaam, Sintah alisema
Diamond alimdhalilisha sana Wema, jambo ambalo si la
kiungwana.
SINTAH AFUNGUKA
“Pamoja na kwamba
wamerudiana, lakini
ukilitafakari tukio lile kwa makini unaweza kuona kabisa
kwamba haikuwa akili ya
Diamond peke yake. Lazima
kuna mtu alikuwa
akimshauri. Haiwezekani mtu
uwe na mapenzi ya dhati kwa mwenzako kiasi cha kufikia
hatua ya kumvalisha pete ya
uchumba, halafu ghafla
unabadili mawazo.
“Haiingii akilini hata kidogo.
Kitendo alichokifanya ni cha kinyama sana. Najua ni kiasi
gani Wema alichanganyikiwa,
ile ilikuwa aibu kubwa sana
kwake. Kuvishwa pete
ukumbini mbele ya
kadamnasi ya watu, halafu siku chache unaachwa...lazima
uchanganyikiwe.
“Nasikia alifikia hatua ya
kutaka kunywa sumu, hiyo
ni kutokana na kuwaza
namna ambavyo angeanza maisha mapya bila Diamond.
Angeweka wapi uso wake?
Hata kama angekuwa nani,
lazima angechanganyikiwa tu.
Mimi nawachukia sana
wanaume wenye tabia kama hii, maana ni vigeugeu na
hawana msimamo.
“Nimetafakari sana, ni kosa
gani kubwa ambalo Wema
alimfanyia kiasi cha kuamua
uamuzi mzito kama ule, lakini nimekosa majibu. Ni nini
kikubwa ambacho kilimfanya
awaite waandishi na
kuwaambia eti anamwaga? Ni
sifa za kijinga tu hizo.
Kuumizana na kupeana presha zisizo na maana. Yaani
alinikera sana.”
AKUMBUSHA YA JUMA
NATURE
Akienda mbali zaidi, Sintah
alisema tukio hilo linamkumbusha ‘sheshe’ lake
na mpenzi wake zilipendwa,
mwana-Bongo Fleva Juma
Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’
ambaye alimpiga chini wakati
akiwa katika penzi zito. “Ndiyo zao hawa wasanii wa
Bongo Fleva, wanasafiria
nyota za wenzao. Wakiona
wamepwaya haraka
wanatafuta wasanii wa
filamu na kutangaza kutoka nao, wanajua lazima magazeti
yataandika, mwisho
wanawabwaga.
“Nasema hivyo nikiwa na
mfano wa kweli, nani
hakumbuki ishu yangu na Juma? (Nature). Ni kawaida
yao, yaani sitaki hata
kukumbuka,” alisema Sintah.
Akishibisha hoja yake, Sintah
alisema ili kuthibitisha
kwamba Diamond hakufanya yale kwa uamuzi wake bali ni
shinikizo, aliweza kurudiana
na Wema kabla hata ya wiki
kupita.
“Hapo kuna mambo mawili,
ushauri kutoka kwa marafiki wabaya au yeye mwenyewe
kuamua kumuacha baada ya
kuona nyota yake imeng’ara.
Tujiulize, aliwezaje kumrudia
haraka haraka, kama yale
yalikuwa maamuzi yake?” alisema Sintah kwa mtindo
wa kuuliza na kuongeza:
“Ni vyema wasichana
wenzangu tukawa makini na
wanaume hasa maarufu
ambao wanataka kung’ara kupitia migongo ya wengine.”
PONGEZI LAKINI...
Pamoja na kutoa makavu bila
kukwepesha, Sintah ametoa
pongezi kwa Diamond kwa
uamuzi wa kurudisha moyo na kumkaribisha tena Wema
mikononi mwake.
“Hilo ndilo jambo la maana
alilofanya. Naamini sasa hata
kama alikuwa na dhamira
mbaya ya kumdhalilisha, atakuwa amegundua
umuhimu wa Wema katika
maisha yake. Unajua huwezi
kuzuia mapenzi ya kweli,”
alisema.
USHAURI WA BURE “Lakini mimi nawashauri
watulie, huu si wakati wa
kuanza kumtafuta mchawi. Ni
vyema wakaangalia maisha
yao ya baadaye. Wao ndiyo
waliopendana na wao wenyewe ndiyo
waliotongozana, hivyo basi
wasimpe mtu nafasi katika
penzi lao.
“Diamond anatakiwa
kufahamu kwamba yeye kama mwanaume, anapaswa
kuwa na msimamo katika
kutoa maamuzi na kuepuka
kusikiliza maneno ya watu
ambayo kwa kiasi kikubwa
ndiyo yanayochangia mifarakano katika mapenzi.”
Oktoba Pili, mwaka huu
Diamond alimfanyia Wema
‘sapraizi’ kwa kumvalisha
pete ya uchumba, tukio
lililochukua nafasi Club Maisha, Masaki, Dar wakati msanii
huyo akipiga shoo ukumbini
hapo katika siku yake hiyo
ya kuzaliwa.
Hata hivyo, kabla wiki
haijakatika, Diamond aliita waandishi wa habari wa
magazeti pendwa na
kutangaza kummwaga, lakini
siku mbili tu baadaye
akaamua kumrudia tena kwa
madai kwamba wamemaliza tofauti zao..

Post a Comment

 
Top