Siku chache baada ya msanii
wa filamu Bongo, Salma Jabu
‘Nisha’ kutangaza kuwa
hajawahi ‘kuduu’ na
mwanaume tangu azaliwe,
baadhi ya wadau wamemchana wakieleza
kuwa, ameongea pumba.
Wakizungumza na Ijumaa
katika nyakati tofauti baadhi
ya watu hao walisema kuwa,
wapo watu wanaoweza kusimama na kusema ni bikira
lakini siyo Nisha.
“Eti bado ana usichana wake,
huko si kutudanganya wazi
wazi? Labda atuambie hao
wanaume ambao tunajua amekuwa akitembea nao
amekuwa akiwaridhisha kwa
njia gani,” alisema Salum wa
Kariakoo.
Naye Janeth wa Mtoni Kwa
Aziz Ally alisema kuwa, Nisha asitake kuwafanya mashabiki
wake ni watoto kwani
wanajua kwa umri wake na
staili ya maisha yake hawezi
kuwa bikira.
Akizungumza na Ijumaa kuhusu kuchanwa huko,
Nisha alisema anasisitiza kuwa
hajaguswa bado na kama
kuna mwanaume aliyewahi
kumuingiza kwenye
ulimwegu wa mapenzi ajitokeze.

Post a Comment

 
Top