Mastaa kiwango katika tasnia
ya Filamu Bongo, Steven
Kanumba na Ivon-cherry
Ngatikwa ‘Monalisa’ hivi
karibuni wamenaswa nchini
Ghana wakila bata. Chanzo chetu ambacho kipo
nchini humo kililitumia gazeti
hili barua pepe inayoeleza
kuwa, wawili hao
wamekuwa wakionekana
maeneo flani ya Jiji la Acra wakiwa pamoja.
“Mona na Kanumba wako
huku wanakula bata kama
hawana akili nzuri ila sijajua
kilichowaleta,” ilisema sehemu
ya barua pepe hiyo. Baada ya kupatikana kwa
maelezo hayo, baadaye
ilibainika kuwa mastaa hao
wapo nchini humo kwa
maandalizi ya kucheza filamu
itakayowashirikisha wasanii kutoka Ghana, Nigeria na
Afrika Kusini.
Kanumba aliposti maelezo
kwenye blog yake kuhusiana
na ziara yao nchini Ghana
akisema: “Tuko huku tunarekodi trela ya filamu
itakayorekodiwa mwakani.
Ni filamu ya Kiafrica
inayorekodiwa barani Afrika
katika maeneo tofauti
yakiwemo Ghana, Dubai na Afrika Kusini.
“Pia itavuka mipaka hadi New
York, Marekani ila mengine
yote yanayobaki ni kutoka
Hollywood. Kwa Bongo ni
mimi na Monalisa tu tutakaoshiriki"

Post a Comment

 
Top