Mwanamziki anaye kimbiza kunako bongo fleva anayejulikana kwa jina la Darasa amemaliza kushoot filamu yake iitwayo Sikati Tamaa.
Sikati Tamaa ni jina la wimbo wake pia aliofanya na Ben Pol na baadaye kufanya remix yake aliowashirikisha Godzilla na Joh Makini.
Akizungumza na Clouds FM leo, rapper huyo amesema filamu yake imefanywa na kampuni ya AM Film Company yenye studio ya muziki ya AM Records.
Pamoja na yeye mwenyewe, mastaa wengine walioshiriki kwenye video hiyo ni pamoja na Adam Mchomvu(BAB JONII), Godzilla, Dj Choka na Madee kutoka TIP TOP.

Post a Comment

 
Top