+lindaikejiblog.jpg)
Taarifa ambayo kila aliekua karibu na Goldie kwenye page
zake za facebook na twitter inakua ngumu kuamini, taarifa rasmi zimeripoti
kwamba Goldie ambae ni mwakilishi wa Nigeria kwenye BBA 2012 AMEFARIKI muda
mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria akitokea Marekani Daktari kutoka Marekani
Reddington Hospital amethibitisha kifo cha Goldie na kusema
chanzo cha kifo chake ni kuziba kwa mishipa wa damu (atery ya mapafu) ambayo imesababishwa na
kuganda kwa damu katika mshipa wa damu kwa lugha ya kitaalamu Coronary Artery
ambapo kwa lugha ya kiatalaamu unaitwa Pulmonar embolism.
Mpenzi wake Goldie ambae ni Msanii wa Kenya CMB Prezzo
ametua Nigeria usiku huu muda mfupi uliopita kwa ajili ya kuendeleza mipango
aliyokua nayo na Goldie ikiwemo kutengeneza show ya TV.
Prezzo alitakiwa kushiriki katika TV show ambayo yeye na
Goldie wangekua moja ya wahusika wakuu ambapo mpango ulikua baada ya mwezi
mmoja Goldie na Prezzo wangekuja Tanzania, Uganda na Kenya kwa ajili ya kujitangaza
na kuipromote single mpya ya Goldie ya ‘Skibobo’ aliyofanya na Ay.
REST
IN PEACE GOLDIE
Post a Comment